Nenda kwa yaliyomo

Rasi ya Italia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 14:45, 5 Machi 2013 na Makecat-bot (majadiliano | michango) (r2.6.5) (Roboti: Imeongeza la:Paeninsula Italiana)
Rasi ya Italia inavyoonekana kutoka angani

Rasi ya Italia au Rasi ya Apenini ni kati ya rasi kubwa za Ulaya yenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,000 kutoka milima ya Alpi hadi kuishia katikati ya Mediteranea.

Iko katika kusini ya Ulaya ikizungukwa na Bahari Mediteranea pande tatu. Umbo la lake ni kama mguu unaocheza mpira na mpira ni kisiwa cha Sisilia.

Karibu eneo lake lote ni nchi ya Italia. Maeneo mawili madogo ndani yake ya kujitegemea ni San Marino na Mji wa Vatikani.

Jina la pili la Rasi ya Apenini latokana na milima ya Apenini inayovuka sehemu kubwa ya urefu wa rasi. Kaskazini kuna tambarare kubwa lenye rutba.

Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.