Nenda kwa yaliyomo

Mwaka wa Kanisa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 6: Mstari 6:


Sikukuu kadhaa kama [[Krismasi]] zinafuata [[tarehe]] za kudumu za [[kalenda ya jua]] lakini nyingine kama [[Pasaka]] tarehe zake zinazosogezwa katika kalenda ya kawaida hasa kwa sababu zinafuata hesabu ya [[Jumapili]] si tarehe katika mwezi fulani.
Sikukuu kadhaa kama [[Krismasi]] zinafuata [[tarehe]] za kudumu za [[kalenda ya jua]] lakini nyingine kama [[Pasaka]] tarehe zake zinazosogezwa katika kalenda ya kawaida hasa kwa sababu zinafuata hesabu ya [[Jumapili]] si tarehe katika mwezi fulani.

Mwendo wa vipindi vya liturujia unafanana na ule wa [[maisha]] ya [[binadamu]], ambayo yana maadhimisho ya pekee na majira ya kukua na kukomaa kwa [[utulivu]]. Vivyo hivyo mwaka wa Kanisa una sikukuu na [[siku za kawaida]], vipindi vya pekee na la. Sehemu muhimu zaidi ya mwaka inategemea [[Pasaka]] na [[Noeli]], sherehe kuu mbili zinazoendesha [[muda mtakatifu]] wote, ingawa zimo sikukuu nyingine pia.


==Mwaka wa kanisa na madhehebu==
==Mwaka wa kanisa na madhehebu==

Pitio la 09:01, 8 Oktoba 2012

Mwaka wa Kanisa kadiri ya kalenda ya liturujia ya Roma kama kielelezo cha kawaida kwa Wakristo wa magharibi.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Mwaka wa Kanisa (pia: mwaka wa liturgia / liturujia) ni mpangilio wa maadhimisho au kalenda inayoratibu majira na sikukuu za Ukristo katika muda wa mwaka 1.

Kalenda hii inataja nafasi ya vipindi kama vile Majilio (Adventi) au Kwaresima, na pia nafasi ya sikukuu.

Sikukuu kadhaa kama Krismasi zinafuata tarehe za kudumu za kalenda ya jua lakini nyingine kama Pasaka tarehe zake zinazosogezwa katika kalenda ya kawaida hasa kwa sababu zinafuata hesabu ya Jumapili si tarehe katika mwezi fulani.

Mwendo wa vipindi vya liturujia unafanana na ule wa maisha ya binadamu, ambayo yana maadhimisho ya pekee na majira ya kukua na kukomaa kwa utulivu. Vivyo hivyo mwaka wa Kanisa una sikukuu na siku za kawaida, vipindi vya pekee na la. Sehemu muhimu zaidi ya mwaka inategemea Pasaka na Noeli, sherehe kuu mbili zinazoendesha muda mtakatifu wote, ingawa zimo sikukuu nyingine pia.

Mwaka wa kanisa na madhehebu

Si madhehebu yote yanaangalia hesabu ya mwaka wa kanisa kwa jumla, lakini karibu zote zinaadhimisha siku kubwa kama Krismasi, Ijumaa Kuu na Pasaka kufuatana na utaratibu wake.

Kimsingi kuna mahesabu mawili:

  1. mapokeo ya magharibi kwa Kanisa Katoliki la Kilatini na Waprotestanti wengi, kama vile Anglikana, Walutheri, Wapresbiteri, Wamoravian;
  2. mapokeo ya mashariki kwa makanisa ya Waorthodoksi na ya Waorthodoksi wa mashariki;
  3. makanisa ya kale ya mashariki pengine huwa na sikukuu na vipindi maalumu (kwa mfano Wakopti na Kanisa la Uhabeshi wanaozingatia hasa sherehe za Bikira Maria).

Tofauti kati ya mapokeo ya magharibi na mashariki kimsingi ni matengenezo ya kalenda ya Juliasi kuwa kalenda ya Gregori; Kanisa Katoliki na Waprotestanti wamepokea kalenda ya Gregori lakini Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda ya Juliasi iliyotangulia.

Muundo wa mwaka wa kanisa

Muundo wa kalenda hii ya mwaka wa kanisa unasimama juu ya sikukuu kubwa mbili za Krismasi na Pasaka na vipindi vya siku vinavyofuatana nazo.

Hesabu hii inaanza na Jumapili ya kwanza ya Majilio (Adventi) katika mapokeo ya magharibi ambayo ni hesabu ya kwawaida kwa Wakristo wengi wa Afrika ya Mashariki. Mwisho wa mwaka wa kanisa ni Jumamosi kabla ya Majilio. Jumapili inayotangulia katika madhehebu mbalimbali inasheherekewa kama sikukuu ya kutazama milele au kurudi kwake Yesu Kristo kama mfalme na hakimu.

Krismasi na kipindi chake inategemea tarehe yake ya 25 Disemba (magharibi) au 6 Januari (mashariki). Jumapili ya nne (au ya sita) kabla ya Krismasi ni mwanzo cha kipindi cha kujitayarisha kwa sikukuu hiyo. Mwisho wa kipindi cha Krismasi ni moja ya Jumapili (au Jumatatu) baada ya Epifania.

Kipindi cha Pasaka kinabadilika tarehe kila mwaka kwa sababu Pasaka yenyewe inategemea hesabu ya Jumapili pamoja na kutazama jua na mwezi yaani aina mbili tofauti za kalenda: ni Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza unaotokea baada ya sikusare ya 21 Machi. Ijumaa Kuu ambayo inaadhimisha ukumbusho wa kifo cha Yesu ni Ijumaa kabla ya Pasaka.

Siku 40 kabla ya Pasaka ni kipindi cha Kwaresima kwa ajili ya maandalizi ya kumbukumbu hiyo ya kusulibiwa na kufufuka kwake. Lakini hesabu ya siku 40 kwa kawaida inaacha Jumapili za kipindi hiki. Ndiyo sababu Kwaresima inaanza kwenye Jumatano kabla ya Jumapili ya sita kabla ya Pasaka, isipokuwa huko Milano na parokia zinazofuata mapokeo yake nchini Italia na Uswisi.

Kipindi cha Pasaka kinakwisha kwenye Jumapili ya Pentekoste[1]; Pentekoste (maana ya neno ni "hamsini", kwa kuwa inatokea takriban siku 50 baada ya Jumapili ya Pasaka).

Vipindi vingine kati ya vipindi vya Krismasi na Pasaka ni majira bila tabia maalumu, lakini kuna sikukuu za kimadhehebu zinazoweza kutofautiana kati ya kanisa na kanisa.

Maana ya mwaka wa kanisa

Ufuatano wa sikukuu unatunza kumbukumbu ya matukio muhimu katika maisha ya Yesu jinsi yanavyosimuliwa katika Biblia ya Kikristo, na pengine hata ya matukio ya historia ya Kanisa, hasa kwa Waorthodoksi.

Wakati dunia inapozunguka kandokando ya jua hadi kurudi ilipokuwa, jumuia ya wafuasi wa Yesu inazunguka kandokando yake ili kuzidi kumfahamu kwa imani, kumuadhimisha kwa tumaini na kumfuata kwa upendo.

Marejeo

  1. Makanisa mengine yanaendelea hesabu yake hadi Jumapili ya Utatu ambayo ni jumapili baada ya Pentekoste

Viungo vya nje