Nenda kwa yaliyomo

Pikipiki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 17: Mstari 17:
==Uwezo wa pikipiki==
==Uwezo wa pikipiki==
Kwa kawaida pikipiki huendeshwa na mtu mmoja lakini inaweza kuchukua pia abiria mmoja1 au wawili ingawa ni 1 tu anayeruhusiwa . Pikipiki inaweza kusafirisha hata mizigo midogo. Kuna pia mabehewa ya kando yanayoongezwa kando la pikipiki au trela inayovutwa nayo.

== Aina za pikipiki ==
Pikipiki za barabara sawa (street motorcycle)--muundo wa pikipiki hizi huziwezesha kutumia barabara za lami

Pikipiki za barabara za vijijini (off-road bike)--hizi huweza kutumia barabara zisizo na ukarabati

Pikipiki za barabara zote(dual bikes)--hizi huweza kutumia barabara za lami au za vijiji.

==Pikipiki na motokaa==
==Pikipiki na motokaa==
Mstari 30: Mstari 37:
* katika nchi zilizoendelea watu wenye motokaa hutumia pikipiki mara nyingi kwa burudani au michezo.
* katika nchi zilizoendelea watu wenye motokaa hutumia pikipiki mara nyingi kwa burudani au michezo.

== Historia ya Pikipiki ==
Pikipiki ya kwanza iliyotumia petroli na mfumo wa internal combusion iliitwa Daimler Raitwagen na ilitengenezwa na Wajerumani wawili kwa jina Gottlieb Daimler na Wilhelm Maybach mwakani 1885 nchini Ujerumani.

Vita vya kwanza vya dunia(First World War) vilichangia pakubwa katika uboreshaji wa pikipiki. Wanajeshi waliona kuwa walikuwa wakitumia muda mrefu sana kusafiri kwa miguu au farasi na kwa hivyo, mahitaji ya pikipiki yakaweza mengi. Kampuni ya Harley-Davidson ilijipata ikitumia takribani asilimia hamsini ya wakati wake katika kutengeneza pikipiki za wanajeshi waliokuwa kwenye vita.

== Pikipiki za leo ==
Hivi leo, utengenezaji wa pikipiki umechukuliwa sana na Wahindi pamoja na Wajapani. Nchi za Afrika na Asia zimekuwa zikinunua pikipiki kwa wingi kwa minajili ya usafiri haswa kwenye barabara zisizo lami, zenye mawe ambako magari hayawezi yakapenya. Hizi [https://www.tigitmotorbikes.com/dirt-bike-tours/ dirt bike tours] huweza kusafiri kwa hali tata, kutumia mafuta yasiyo mengi na kupenya vijijini visivyo na barabara zenye ukarabati.

[[Category:Usafiri| ]]
[[Category:Usafiri| ]]

Pitio la 11:06, 28 Septemba 2018

Watu wawili juu ya pikipiki nchini Uhindi
Pikipiki ya Kirusi yenye behewa ya kando
Pikipiki ya michezo wakati wa mashindano ya mbio

Pikipiki ni chombo cha usafiri chenye magurudumu mawili kinachoendeshwa kwa nguvu ya injini ama ya mwako ndani au ya umeme.

Chanzo cha pikipiki ilikuwa baisikeli iliyoongezwa injini.

Injini

Pikipiki ndogo huwa mara nyingi na injini ya mapigo mawili lakini kubwa huwa na injini za mapigo manne. Mara nyingi ni injini za petroli kuna pia za diseli. Injini za umeme zimeanza kutumiwa juzijuzi tu zinaenea polepole katika nchi zilizoendelea.

Nguvu ya injini hupelekwa kwenda gurudumu la nyuma kwa njia ya mnyororo. Pikipiki kubwa huwa pia na mhimili kutoka injini hadi gurudumu la nyuma.

Uwezo wa pikipiki

Kwa kawaida pikipiki huendeshwa na mtu mmoja lakini inaweza kuchukua pia abiria mmoja1 au wawili ingawa ni 1 tu anayeruhusiwa . Pikipiki inaweza kusafirisha hata mizigo midogo. Kuna pia mabehewa ya kando yanayoongezwa kando la pikipiki au trela inayovutwa nayo.

Aina za pikipiki

Pikipiki za barabara sawa (street motorcycle)--muundo wa pikipiki hizi huziwezesha kutumia barabara za lami

Pikipiki za barabara za vijijini (off-road bike)--hizi huweza kutumia barabara zisizo na ukarabati

Pikipiki za barabara zote(dual bikes)--hizi huweza kutumia barabara za lami au za vijiji.

Pikipiki na motokaa

Pikipiki zilijitokeza wakati ule kama motokaa. Mtu mmoja husafiri kwa gharama kidogo kwa pikipiki kuliko kwa gari. Tofauti na magari pikipiki haina kinga dhidi ya mvua, baridi au joto kali. Lakini pikipiki ni nyepesi na kwa sababu hiyo huwa na mbio kushinda motokaa. Hata hivyo ni hatari zaidi kuitumia kwa sababu dereva hana kinga dhidi ya ajali. Kwa sababu hiyo kuna nguo za kinga kama kofia ya pikipiki na nyingine.

Matumizi ya Pikipiki

Kimsingi pikipiki hutengenezwa kwa kumbeba dereva pamoja abiria 1.

  • Boda boda za pikipiki hubeba abiria kama teksi.
  • Pikipiki hutumiwa hasa mjini kubeba mizigo midogo kama spea au barua kati ya ofisi na maduka.
  • migahawa yenye huduma ya kuwapelekea wateja chakula hadi nyumbani husafirisha mara nyingi kwa pikipiki wakipokea maagizo kwa njia ya simu.
  • wakulima wasio na uwezo wa kununua gari hubeba mazao hadi sokoni.
  • katika nchi zilizoendelea watu wenye motokaa hutumia pikipiki mara nyingi kwa burudani au michezo.

Historia ya Pikipiki

Pikipiki ya kwanza iliyotumia petroli na mfumo wa internal combusion iliitwa Daimler Raitwagen na ilitengenezwa na Wajerumani wawili kwa jina Gottlieb Daimler na Wilhelm Maybach mwakani 1885 nchini Ujerumani.

Vita vya kwanza vya dunia(First World War) vilichangia pakubwa katika uboreshaji wa pikipiki. Wanajeshi waliona kuwa walikuwa wakitumia muda mrefu sana kusafiri kwa miguu au farasi na kwa hivyo, mahitaji ya pikipiki yakaweza mengi. Kampuni ya Harley-Davidson ilijipata ikitumia takribani asilimia hamsini ya wakati wake katika kutengeneza pikipiki za wanajeshi waliokuwa kwenye vita.

Pikipiki za leo

Hivi leo, utengenezaji wa pikipiki umechukuliwa sana na Wahindi pamoja na Wajapani. Nchi za Afrika na Asia zimekuwa zikinunua pikipiki kwa wingi kwa minajili ya usafiri haswa kwenye barabara zisizo lami, zenye mawe ambako magari hayawezi yakapenya. Hizi dirt bike tours huweza kusafiri kwa hali tata, kutumia mafuta yasiyo mengi na kupenya vijijini visivyo na barabara zenye ukarabati.