Nenda kwa yaliyomo

Pikipiki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2) (roboti Nyongeza: ta:விசையுந்து
d r2.6.4) (roboti Nyongeza: mn:Мотоцикл
Mstari 74: Mstari 74:
[[mk:Мотоцикл]]
[[mk:Мотоцикл]]
[[ml:മോട്ടോർ സൈക്കിൾ]]
[[ml:മോട്ടോർ സൈക്കിൾ]]
[[mn:Мотоцикл]]
[[ms:Motosikal]]
[[ms:Motosikal]]
[[nl:Motorfiets]]
[[nl:Motorfiets]]

Pitio la 17:24, 4 Januari 2012

Watu wawili juu ya pikipiki nchini Uhindi
Pikipiki ya Kirusi yenye behewa ya kando
Pikipiki ya michezo wakati wa mashindano ya mbio



Pikipiki ni chombo cha usafiri chenye magurudumu mawili kinachoendeshwa kwa nguvu ya injini ama ya mwako ndani au ya umeme.

Chanzo cha pikipiki ilikuwa baisikeli iliyoongezwa injini.

Injini

Pikipiki ndogo huwa mara nyingi na injini ya mapigo mawili lakini kubwa huwa na injini za mapigo manne. Mara nyingi ni injini za petroli kuna pia za diseli. Injini za umeme zimeanza kutumiwa juzijuzi tu zinaenea polepole katika nchi zilizoendelea.

Nguvu ya injini hupelekwa kwenda gurudumu la nyuma kwa njia ya mnyororo. Pikipiki kubwa huwa pia na mhimili kutoka injini hadi gurudumu la nyuma.

Uwezo wa pikipiki

Kwa kawaida pikipiki huendeshwa na mtu mmoja lakini inaweza kuchukua pia abiria mmoja1 au wawili ingawa ni 1 tu anayeruhusiwa kusheria. Pikipiki inaweza kusafirisha hata mizigo midogo. Kuna pia mabehewa ya kando yanayoongezwa kando la pikipiki au trela inayovutwa nayo.

Pikipiki na motokaa

Pikipiki zilijitokeza wakati ule kama motokaa. Mtu mmoja husafiri kwa gharama kidogo kwa pikipiki kuliko kwa gari. Tofauti na magari pikipiki haina kinga dhidi ya mvua, baridi au joto kali. Lakini pikipiki ni nyepesi na kwa sababu hiyo huwa na mbio kushinda motokaa. Hata hivyo ni hatari zaidi kuitumia kwa sababu dereva hana kinga dhidi ya ajali. Kwa sababu hiyo kuna nguo za kinga kama kofia ya pikipiki na nyingine.

Matumizi ya Pikipiki

Kimsingi pikipiki hutengenezwa kwa kumbeba dereva pamoja abiria 1.

  • Boda boda za pikipiki hubeba abiria kama teksi.
  • Pikipiki hutumiwa hasa mjini kubeba mizigo midogo kama spea au barua kati ya ofisi na maduka.
  • migahawa yenye huduma ya kuwapelekea wateja chakula hadi nyumbani husafirisha mara nyingi kwa pikipiki wakipokea maagizo kwa njia ya simu.
  • wakulima wasio na uwezo wa kununua gari hubeba mazao hadi sokoni.
  • katika nchi zilizoendelea watu wenye motokaa hutumia pikipiki mara nyingi kwa burudani au michezo.